user_mobilelogo

Party Emblem

Party Flag

 

Youth League

Contact us


Communist Party Marxist - Kenya (CPM-K)
This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.
P.O Box 101011-00101 Nairobi, Kenya.
 

Let's Get Social

          

 

Related Social Links

 Revolutionary Youth League (RYL)
   
 Revolutionary Student Commission
    
 Revolutionary Women League
 Pio Gama Pinto Institute 

Support CPM-K 

membership

Publications

 

 

 Grab a Copy

 

CPM-K Memberships

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Nawasalimu Makada wote wa Chama Cha Kimonunisti Kenya na Wageni wote waalikwa. Siku ya leo ambayo ni siku muhimu sana yakuadhimisha na kuwasherehekea wafanyikazi wote duniani. 

Leo tunajumuika hapa Kisumu lakini sisi ni baadhi tu ya wavujajasho wengi waliojumuika katika kila Pembe ya dunia kusherehekea nguvu Kazi ya wavujajasho duniani.

Lakini, Kuna nini  chakusheherekea kwa  wafanyikazi ? Wakati mabilioni ya wafanyikazi wanaendelea kukandamizwa na mfumo wa kiimla wa ubepari. Mfanyikazi hana chochote chakusheherekea katika jamii yenye inaongozwa na  uimla wa mtaji wakibinafsi dhidhi ya maslahi ya wanaotengeneza mtaji huo.

Jamii yetu imegawanyika baina ya wavunajasho wachache wanao miliki nyenzo za uzalishaji na wanaozitumia kunyonya nguvukazi ya wavujajasho wengi ambao wanaendelea kuishi maisha ya kichochole.

Wafanyikazi wa Kenya kama wafanyikazi wengine wameenedelea kukandamizwa kwa kulipwa Mishahara duni na isiyoweza kukimu mahitaji yao, wafanyikazi wameendelea kufanya kazi masaa zaidi ya yale yanayotakikana na sheria za kufanya kazi duniani. Mazingira yakufanya Kazi yamezorota na wafanyikazi wengi wanapata ajali na hata magonjwa kutokana na Mazingira duni yakufanya kazi. 

Serikali ya Kenya haijaweka mikakati yoyote yakulinda maslahi ya wafanyikazi na hata kuongeza nguvukazi ya taifa lenye lina watu waliohitimu katika tajriba tofauti na ambao bado hawajapata kazi kwa sababu yakutoendeleza viwanda na kilimo ambayo ndiyo nguzo msingi ya nchi yeyote inayotaka kujiendeleza.

Mashirika yakimataifa kama Benki ya Dunia na IMF( International Monetary Fund) yameendelea kushinikiza matakwa ya ulibarali mamboleo ambayo yamekua na madhara makubwa kwa wafanyikazi na maisha ya mvujajasho wa Kenya.

Serikali hii ya kiimla pia imeendelea kusimamisha na kupinga juhudi zozote za wafanyikazi kuungana na kujitetea. Polisi wametumika kuwapiga wafanyikazi wakati wanapo fanya migomo na serikali imekataa kufuata mikataba ya makubaliano na wafanyikazi wa umma.

Vyama vya wafanyakazi na viongozi wa vyama hivi pia wamenunuliwa ili kulegeza kamba katika mapambano ya wafanyikazi. Sisi wakomunisti tukona na jukumu lakuenda miongoni  mwa wafanyikazi hawa na kuwapa mwamko Mpya wa kimawazo ili wabadilishe mambo yalivyo.

Sisi wakomunisti tunafaa kuendelea na kazi yakujenga vyama hivi vya wafanyikazi na kuleta mawazo ya kimapinduzi kwa wafanyikazi ili waelewe   uwezo walio nao. 

 Ingawaje,  vyama hivi vingine vimeshikiliwa na mabepari mchwara wanaotumia uongozi wao ili kuendelea kujinufaisha kibinafsi kama katibu mkuu wa COTU(Confederation of Trade Union) Bwana Francis Atwoli. Viongozi hawa ni kupe wanaonyonya jasho la wafanyikazi wakenya na lazima tuwapinge ki itikadi na tuwang'oe ili turejeshe hadhi ya vyama vya wafanyikazi wakati wa wazalendo kama Makhan Singh, Fred Kubai, Bildad Kaggia na Chege Kibacia.

Wakomunisti pia tunajukumu la kujenga Chama cha Kisiasa cha wafanyikazi CPM-K kwani tunapigana kuchukua uongozi na kujenga uimla wa wafanyikazi dhidhi ya wanaomilki mtaji, hii ndio njia yakujenga mfumo wa usoshialisti ili kuelekea katika mfumo wa kikomunisti ambapo hakuna ukandamizaji baina ya binadamu na binadamu mwingine.

Chama Chetu CPM-K ndicho kitapeleka harakati na gurudumu la wafanyikazi mbele ya mambo mengine ambayo vyama vingine vya wafanyikazi haviwezi kutekeleza. 

Makada wote wa Chama wanajukumu la kihistoria na la kijamii kujenga Chama mahali wanapofanyia kazi ili kuleta mawazo yakimapinduzi kwa wafanyikazi wengine, Chama chetu nicha wafanyikazi na lazima tukijenge miongoni mwa wafanyikazi wenyewe.

Chama chetu kitajaribu kuleta pia Wakulima na wavujajasho wengine katika jamii ili kuikomboa Kenya na dunia kutokana na maovu ya ubepari na ubeberu. Mapigano ya kwanza yakatukua dhidhi ya mabepari wa nyumbani wanaoendeleza maslahi ya mabeberu na mabepari wa nje kwa kufanya kazi ya kibaraka na kutumia vyombo vya dola venye vinamilikiwa na mabepari wa nje ili kukandamiza jamii.

Nawatakia mazungumzo yenye fanaka katika mkutano wa leo wakuadhimisha siku hii na tuendele kujenga Chama cha wafanyikazi.

 

Yadumu Mapambano ya wafanyikazi !!!

Idumu harakati za kujenga Usoshalisti!!!

Kidumu Chama Cha Wafanyikazi CPM-K !!!

Mwaivu Kaluka.

Mwenyekiti Wa Chama Cha Kikomunisti Umaksi - Kenya.

THE DRIVE INTO WORLD WAR 3 AND THE WORLD ANTI IMPERIALIST FRONT
11 May 2026 07:14

  ate:  10b>th May 2026 Occasion: International Colloquium by World Anti-Imperialist Platform, Nairobi    Author: Booker Omole Position: General Secretary, Communist Party Marxist Kenya   E DRIVE INTO WORLD WAR 3 AND THE HISTORICAL EPOCH   Comrades, we are not living in ordinary times. We are living in a time of rupture, a time of transition, a time when the old order is decaying but refuses to die, and the new order is struggling to be born. The drive into a Third World War is not an accident. It is not a misunderstanding. It is not the result of individual leaders acting irr [ ... ]

Read more
STATEMENT OF THE COMMUNIST PARTY MARXIST KENYA (CPMK)
11 May 2026 07:14

  O THE WORLD ANTI IMPERIALIST PLATFORM CONFERENCE   NAIROBI, KENYA 14th MAY 2026   LL FOR INTERNATIONAL SOLIDARITY AGAINST REPRESSION, ABDUCTIONS, AND POLITICAL PERSECUTION IN KENYA   Dear comrades, revolutionary delegates, brothers and sisters in struggle,   The Communist Party Marxist Kenya extends militant greetings to all anti imperialist organisations gathered here in Nairobi. We welcome you at a critical moment in the history of Kenya, Africa, and the world anti imperialist movement. This conference is taking place at a time when imperialism is intensifying its aggres [ ... ]

Read more
The National Democratic Revolution in Kenya: Tasks of the Anti imperialist and A...
11 May 2026 07:12

  y Booker Omole General Secretary Communist Party Marxist Kenya   9th May 2026   Presented at the World Anti imperialist Front Theoretical Conference, Nairobi.   Question of Revolution in Kenya Kenya stands at a decisive historical juncture. This is not a moment of calm. This is not a moment of neutrality. This is a moment of sharpening contradictions, of deepening crisis, of rising struggle. The question before us is not whether change will come. The question is what kind of change, led by which class, in whose interests. We must speak plainly. Kenya is not an independent [ ... ]

Read more
LETTER TO THE GLOBAL NORTH
05 May 2026 14:16

 Comrades, We address you at a historical precipice. The global capitalist system, in its advanced stage of heightened imperialism, is characterized by deepening crises and escalating violence. The centers of imperial power—Washington, Brussels, London, Paris are intensifying their efforts to maintain a hegemony that is increasingly contested. In the Global South, we are the primary targets of this aggression. The mechanisms of our oppression are calculated and brutal. We are strangled by illegitimate debt, wielded not as economic aid, but as a weapon of political control by institution [ ... ]

Read more